March 2016

Sheria ya TEITI Imeitaka Serikali Kuweka Mikataba na Majina ya Wamiliki wa Kampuni za Madini na Gesi Asilia Wazi: Mbona Bado ni Siri, Tatizo ni Nini?

Nchi 51wanachama zinazotekeleza Mpango wa EITI (Extractive Industries Transparency Initiative) zilikutanamjiwa Lima, Peru, Marekani ya Kusini kuhabarisha na juu ya maendeleo ya utekelezaji wa Mpango huo kwa kila nchi mwanachama. Mkutano huu wa kimataifa ulifanyika Februari 24-25, 2016 na kuhudhuriwa na watu wanaokadiliwa kuwa 1,400 kutoka nchi 100. Serikaliya Tanzania iliwakilishwanaBalozi wake aliyepo Brazil pamoja na baadhi ya wajumbe kutoka kwenye bodii nayosimamia Mpango wa EITI nchini, yaani Multi-Stakeholder Working Group (MSG).