JET waishauri Serikali kuzingatia Mazingira

Chama cha waandishi wa habari za Mazingira – JET kimeishauri serikali kuzingatia suala la mazingira wakati wa utekelezaji wa uanzishwaji wa viwanda ili kuhakikisha taifa linakuwa na viwanda bora vyenye kujali na kulinda mazingira.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama hicho Dokta ELLEN OTARU wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho ambapo pamoja na mambo mengine wameadhimia kutoa elimu juu ya masuala ya mafuta na gesi kwa waandishi na wahariri wa habari.

Naye mkurugenzi mtendaji wa Chama hicho cha wanahabari JOHN CHIKOMO amesema katika kuhakikisha wanahabari wanakuwa na uelewa wa masuala ya mafuta na gesi watahakikisha wanatoa elimu hiyo kwa waandishi na wahariri.

Nao waandishi wa habari wameishauri jamii kushirikiana nao katika kuibua masuala ya mazingira pamoja na kulinda mazingira.

Chama cha waandishi wa habari za mazingira linajumla ya wanachama Mia Moja Thelathini na Mbili kutoka Tanzania bara na visiwani.

Na Leah Mushi TBC - JET MEMBER
source: http://www.tbc.go.tz/read/?id=IjkxNTUi