Sheria ya TEITI Imeitaka Serikali Kuweka Mikataba na Majina ya Wamiliki wa Kampuni za Madini na Gesi Asilia Wazi: Mbona Bado ni Siri, Tatizo ni Nini?

Nchi 51wanachama zinazotekeleza Mpango wa EITI (Extractive Industries Transparency Initiative) zilikutanamjiwa Lima, Peru, Marekani ya Kusini kuhabarisha na juu ya maendeleo ya utekelezaji wa Mpango huo kwa kila nchi mwanachama. Mkutano huu wa kimataifa ulifanyika Februari 24-25, 2016 na kuhudhuriwa na watu wanaokadiliwa kuwa 1,400 kutoka nchi 100. Serikaliya Tanzania iliwakilishwanaBalozi wake aliyepo Brazil  pamoja na baadhi ya wajumbe kutoka kwenye bodii nayosimamia Mpango wa EITI nchini, yaani Multi-Stakeholder Working Group (MSG).

Mpango wa EITI unalengakuhamashishauwazina uwajibikaji katikakukusanya na kusimamia mapatoyamadini, gesiasilianamafuta ili yasaidie kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa kila raia.

Tanzania ilijiunganaMpangowa EITI mwaka 2009 nakupataCompliance Statusmwaka 2012.NchiinapotunikiwahadhiyaComplianceStatusinamaanishatayariimewekamfumowakutoataarifayamapatokwaummakilamwakaikielezakiasiilichokusanyakutokakwenyesektayarasilimalizamadini, gesiasilianamafuta.  Tanzania haijagunduamafutabado, hivyotaarifazamapatozinazotakiwakutolewakatika taarifa za kila mwaka kwa wananchi nijuu ya mapato ya rasilimali za madininagesiasilia. Tanzania kupitia MSG imetoataarifahizizamapatokutokamadininagesiasiliakuanzia mwaka 2008 hadi 2014. Taarifahizizinapatikana: www.teiti.or.tz

UtekelezajiwaMpangowa EITI nchininautoajiwataarifazamapatoyamadininagesiasiliakilamwakakwamujibuwakanunina utaratibu waEITI nihatuanzurikatikamwelekeowakujengamisingiyautawala bora inayoitakaSerikalikuwajibikakwawananchijuuyamapatonamatumiziyarasilimalizanchi. MafanikioyaMpangowa EITI nchininimatundayakazinzuriya MSG pamojanamsimamowaSerikaliyaAwamuyaNneyaMhe. JakayaKikwetekatikakuhakikishauchimbajiwamadininagesiunaendasambambanauzingatiajiwaMpangowa EITI. Ili kuwezakujenganakuimarishamisingihiiyautawala bora, uwazinauwajibikajikatikausimamiziwauchimbaji madininagesiasilia na mapato yake, SerikaliyaAwamuyaTanoyaMhe. J.P.J. Magufuliinashauriwakuzingatia mambo kadhaayafuatayo:KutumiaSheriayaTanzania Extractive Industries (Transparency and Accountability) ACT, 2015 katikakuhakikishakuna uwazinauwajibikajikatikamapatoyamadininagesiasilia.

Kumekuwepo na tabia nchini kutunga sheria nyingi ambazo zinaenda tu kwenye rundo la orodha ya sheria zilizopo nchini wakati uundaji wa sheria hizi huigharimu sana Serikali ambayo hutumia fedha za walipa kodi. Sheriahiiya TEITI ilipitishwana Bunge Juni 2015 nakusainiwakuwasherianaMhe. RaisMstaafuJakayaKikwete Agosti 2015 sambambanasherianyinginembilizakusimamiasektayagesi asilia: 1) Petroleum ACT, 2015 na 2)Tanzania Oil and Gas Revenue Management ACT, 2015). Sheriahizitatukwapamojaiwapozitatekelezwakwamujibu wamalengoyakezitaisaidiaSerikalikutumiarasilimalizamadininagesiasiliakukuzauchumi wa nchiyetunakupunguzaumasikiniwaWatanzania.Hivyo basi sheria hizi tatu ni vyema zikatumiwa ipasavyo kwani Watanzania wana shauku kubwa ya kuona gesi asilia iliyogunduliwa nchini inasaidia kukwamua Watanzania kutoka kwenye umasikini uliokithiri nchini.

Umaskini huu tunaupima kwa kuzingatia ya kwamba bado Serikali haijaweza kuhakikisha nchini kila kijiji kinakuwa na zahanati, kila kata inakuwa na kituo cha afya, dawa na huduma za afya zinapatikana kwa wakati na bila kusuasua, shule zote za msingi na sekondari zinapata madarasa, nyumba za walimu, madawati na vitabu vya kutosha na watumishi wa sekta za elimu na afya wanalipwa mishahara yao kwa wakati. Miundombinu ya barabara, umeme na maji safi na salama nchini bado ni changamoto kubwa. Kwa kuwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali ni mdogo ukilinganisha na mahitaji haya ya huduma za jamii, Serikali ina kila sababu ya kuhakikisha mapato kutokarasilimali za gesi asilia na madini yanasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto hizi.

Kushuka kwa bei ya mafuta na gesi asilia duniani kisiwe chanzo cha kukata tamaa juu ya uwezo mkubwa wa rasilimali ya gesi asilia kusaidia kukuza uchumi na kupunguza umasikini. Historia ya kupanda na kushuka kwa bei ya mafuta na gesi asilia duniani inatuonesha kwamba bei huwa hazikai chini milele. Wakati tunasubiri bei zipande Serikali ina fursa nzuri hivi sasa kuhakikisha taasisi zinazohusika na kusimamia rasilimali za gesi asilia (na madini) zinajipanga kushirikiana kikamilifu kuisaidia nchi kufikia malengo ya kutumia rasilimali hizi kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

Uchimbaji na usimamizi wa mapato kutoka rasilimali za madini na gesi asilia hukumbana na changamoto za rushwa na ubadhilifu wa fedha za umma hivyo Serikali inapaswa kuhakikisha sheria ya TEITI inasaidia kuiepusha Tanzania kwenda kwenye orodha ya nchi ambazo rasilimali hizi zimenufaisha wachache (mafisadi) na kuacha wananchi wengi kwenye umaskini uliokithiri. Sheriaya TEITI inamaeneomawiliambayoiwapoSerikaliitayatekeleza ipasavyoyatasaidiasanakujengamisingiyauwazi, uwajibikaji na utawala bora katika usimamizi wa mapato ya rasilimali za gesi asilia na madini.

Kifungu cha sheria cha 16 (1) (a) yaSheriaya TEITIinaitakaSerikalikuwekamikatabayamadininagesiasiliawazi. SheriahiiilianzakufanyakazibaadayakusainiwanaMhe. Rais Kikwete, tarehe 25 Septemba, 2015 lakinimpakahivisasaMachi 2016 hakunahatamkatabammojaumeishawekwawazi. Kuwekamikatabawazikunamanufaamakubwakwaummakwani Bunge nawananchikwaujumlawanawezakusomamikatabanakutathiminikamauchimbajinausimamiziwasektazamadininagesiasiliaunatekelezwakwamujibu wa sheria na kamamakubalianokwenyemikataba yanazingatia masilahi ya umma. Kuendeleakufichamikatabakunafanyawananchiwawena mashakanaSerikalihata pale ambapoSerikaliimewekamasilahiyaummambele katikamikatabahiyo. Bilakuwekamikatabawaziwabunge na wananchiwataendelea kujiuliza kuna nini kwenye hii mikataba mbona inafichwa? Waingereza walisema kwamba to see is to believe. KwenyeBiblia Thomas hakuaminikamaYesuamefufukampakaalipoonakwa macho yakenguonasanda la Yesundipoakaamini.

Kifungu cha sheria cha16 (1) (b)yaSheriaya TEITIinaitakaSerikalikuwekawazimajinayawamilikiwakampunizinazojishughulishanauchimbajiwamadininagesiasilianchini.Matakwahayayatasaidiakuondoasirizamajinayawamilikiwakampuni. Baadhi ya kampunihutumia majinahewailikukwepakodi bila kuvunja sheria (throughtransfer price, over-invoicing of imports, under-invoicing of exports, bribery, money laundering, and contract fraud). Aidha, kuweka mikataba na majina ya wamiliki wa kampuni hizo wazi kutasaidia kuondoatabia ya baadhiyawatumishiwaSerikali(politically exposed persons) wasio waaminifu na wazalendo kuihujumu nchi kwa kuangalia masilahi yao binafsi na yale yawawekezaji badala ya kuweka masilahi ya nchi kwanza.

Kwa mujibu wa Sheria ya TEITI leseni ama mikataba iliyosainiwa kuanzia tarehe 25 Septemba, 2015 inatakiwa iwe wazi kwa umma. Kwa mikataba ambayo ilisainiwa kabla ya tarehe tajwanayo inatakiwa kuwekwa wazi ila mpaka hivi sasa ni takribani miezi miezi sita tangu sheria hii imeanza kufanya kazi lakini bado mikataba hii ni siri.

Inatubidi kutumia rasilimali za gesi asilia (na madini) kutusaidia kufikisha malengo ya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. Kwa kufanya hivyondoto na haki ya kila Mtanzania kupata elimu bora, afya bora, barabara bora, umeme na maji safi na salama kwa kila kaya vijijini na mjini ifikapo 2025inawezekana japo mchakato wa kuuza gesi ya kwanza nchi za nje unawezekana ukawa haujawa tayari ifikapo 2025. Kuna makubaliano ya msingi inabidi yafanyike kati ya Serikali na kampuni zilizowekeza kwenye kuchimba gesi asilia ndipo kampuni ziamue mwaka ambao wataanza uchimbaji wa gesi asilia iliyopo kwenye kina kirefu cha Bahari ya Hindi.

Iwe ni kabla ya 2025 ama baada ya hapo, rasilimali ya gesi asilia (na madini) ina nafasi kubwa sana ya kuleta mabadiliko ya uchumi na kusaidia kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania. Ili mabadiliko haya yaweze kuwepo inaibidi Serikali iendelee kuimarisha misingi ya utawala bora, kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji katika kusimamia rasilimali za nchi. Serikali itumie Sheria ya TEITI sambamba na sheria nyingine kuhakikisha haya mageuzi ya kiuchumi na kijamii yanapatikana. Usiri wa mikataba ya rasilimali za madini na gesi asilia nalo ni jipu la muda mrefu inabidi litumbuliwe haraka iwezekanvyo. Sheria ya TEITI imeundwa kwa ajili ya hiyo kazi, Serikali inasubiri nini?