Shirika lisilo la kiserikali la Hivos Afrika Mashariki (Hivos East Africa) na kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Africa Ltd kwa kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa Habari Wa Mazingira (JET) wanayo furaha kuanzisha mafunzo maalum ya wanahabari kwa vitendo katika masuala ya nishati jadidifu (Renewable energy reporting) ili kuzalisha habari za nishati zenye mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa na kwa vyombo habari husika.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kati ya mwezi Desemba 2019 na Mei 2020. Wanahabari watakaochaguliwa pia watakuwa na fursa ya kuhudhuria kambi maalum ya nishati kwa wanahabari (Renewable Energy Bootcamp) kwa siku tatu huko Dodoma. Kambi hiyo itafanyika kati ya Novemba 12 - 14, 2019 na itaratibiwa kwa ushirikiano na washirika wengine ikiwa na dhumuni la kuunganisha wadau mbalimbali kwa ajili ya maendeleo endelevu ya nishati.

Gharama za mafunzo hayo zitalipiwa na waandaaji. Ili kuhakikisha maarifa yatakayopatikana katika mafunzo hayo yanatumika ipasavyo, wanahabari watapatiwa ruzuku ya kuwawezesha kufanya uchunguzi wa kihabari katika maeneo watakayochagua na kuzalisha habari zilizofanyiwa utafiti wa kina kuhusu nishati jadidifu baada ya mawazo yao kupitishwa na wakufunzi wao.

Tunapenda kufahamu zaidi wasifu wako na nia ya kujiunga na mafunzo hayo. Usaili wa washiriki utazingatia motisha uliyonayo. Pia, usawa wa kijinsia, taaluma, aina ya chombo cha habari na eneo unalotokea vitazingatiwa. Muombaji anapaswa kuwa na umri kati ya miaka 18 na 50.

Kwa swali lolote kuhusu maombi ya kujiunga na mafunzo haya, tafadhari wasiliana na Daniel Mwingira kupitia danny@nukta.co.tz au kwa njia ya simu +255 716 731 383; Mercy Masinga kupitia simu ya mkononi +25743194414 na Caroline Manyama kupitia simu ya mkononi +255 629 144 989 au barua pepe jetassociation@gmail.com.

Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi: Oktoba 18, 2019 Saa 5:59 usiku.

Unaweza kutufuata katika mitandao ya kijamii: Twitter: @nuktaTanzania, @NuktaAfrica, @ hivosroea, @AssociationTz | Facebook: NuktaTanzania, | Tovuti: www.nukta.co.tz na https://east-africa.hivos.org.

N.B: Taarifa hizi ni kwa ajili ya matumizi ya kufanikisha usaili wa mafunzo haya tu wala hazitatumika vinginevyo.


English version

Hivos East Africa and Nukta Africa in collaboration with Journalists Environmental Association of Tanzania (Jet) are delighted to conduct a Renewable Journalists Energy Fellowship program which aim at building capacity of journalists in Tanzania to produce high quality renewable energy stories with impact to the nation and their respective media houses.

The program will run between December 2019 and May 2020. The selected journalists will also have an opportunity to attend Renewable Energy Bootcamp for three days in Dodoma. The bootcamp, a curtain raiser to renewable energy fellowship, will take place in Dodoma from 12th - 14th November 2019 in collaboration with others partners.

Organizers will cover all costs to attend the training. Field trip grant will be provided solely to cover investigative renewable energy stories in areas selected by journalists after recommendations from mentors.

We would like to learn a bit more about you: What is your background and why you are interested on the bootcamp and the renewable energy fellowship?

We will select our participants based on motivation and we strive for a fair balance in gender, academic and professional backgrounds. Applicants must be aged between 18 and 50.

If you have any questions about the application process, please contact:-

Daniel Mwingira; email danny@nukta.co.tz or via phone +255 716 731 383; Mercy Masinga via +25743194414 or Caroline Manyama via phone +255 629 144 989 and email jetassociation@gmail.com.

Application deadline: 18th October 2019 at 23:59.

Follow us: Twitter:@nuktaTanzania, @hivosroea | Facebook:Nukta, @AssociationTz | Website: www.nukta.co.tz and www.jet.org

#REJF 2.0 #WaandishiNishati

N.B: The information (data) extracted in this form are solely for the selection process and won't be transferred or used otherwise.

 

Click on Link below to fill online:

https://docs.google.com/forms/d/1bJjnMLIt_qJlbzpY6UPDjMRS4pK5BDmG5NjtPS6PM0I/viewform?edit_requested=true&edit_requested=true