SERA YA TAIFA YA ARDHI YA 1995

Sera hii inaweka kanuni za msingi zinazotawala mfumo mzima wa umiliki, usimamizi na matumizi ya ardhi nchini. Kanuni hizo ni pamoja na:-

· Kutambua kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya umma na kuwa imewekwa mikononi mwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya raia wote.

· Kulipa fidia kamili, ya haki na kwa wakati kwa mtu yeyote ambaye haki miliki inafutwa matumizi yake.Pia kuwezesha ardhi kugawiwa kwa haki na kupatikana kwa raia wote

· Kuwawezesha raia wote kushiriki katika kutoa maamuzi ya mambo yanayohusiana na milki au matumizi yao ya ardhi.

· Haki ya kila mwanamke kupata,kumiliki,kutumia na kuuza au kuigawa ardhi kuwa sawa na haki ya mwanaume yeyote kwa viwango na masharti sawa